Storm FM

Acheni kufugia kuku vyandarua jikingeni

1 May 2021, 12:12 pm

Na Kale Chongela:

Wakazi wa mtaa wa Msalalaroad kata ya kalangalala Halmashauri ya mji wa Geita  wameshauriwa  kuendelea kuzingatia matumizi ya vyadarua ili kujikinga na mbu waenezao malaria nasiyo kuvitumia kwa matumizi mengine ikiwemo kufugia mifugo.

Rai hiyo imetolewa na  mtoa huduma za afya ngazi ya jamii katika Mtaa huo Bi Jetruda  John  wakati akifanya tathimini  ya matumizi bora ya vyadarua   nakubainisha kuwa  licha ya Elimu kuendelea kutolewa lakini bado jamii imekuwa ikijisahau kutumia vyadarua.

Mtoa Huduma za Afya

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wametumia fursa hiyo  kuiomba serikali kuendelea kutoa elimu  mara kwa mara juu ya mwenendo wa hali ya malaria mkoani Geita.

Mwenyekiti wa serikalia ya Mtaa  huo BW Sostenes karist amesema  wamekuwa wakitumia mikutano ya mtaa kutoa elimu ya matumizi bora ya vyandarua.