Storm FM

Uislam wazungumzia lishe na virutubisho

10 July 2023, 8:11 pm

Dr. Khalid Hussein kutoka taasisi ya Utafiti na Ugunduzi ya TABCCOM Herbal Research Center and Rescue Community Wellbeing Tanzania akiwa Geita na kuzungumzia umuhimu wa lishe bora. Picha na Said Sindo.

Suala la kufuata utaratibu wa mlo kamili ni la muhimu ili kuimarisha afya, ili kutimiza azma ya serikali kuandaa wataalam wabunifu wa kizazi kinachokuja, viongozi mbalimbali wa kiserikali na kiimani wameendelea kusisitiza kuwa lishe si suala la hiari, wanaowaza hivyo waache mara moja na watekeleze kama ilivyo maelekezo na malengo ya serikali kuwa na jamii yenye lishe bora na kwa kujenga afya zao.

Na Said Sindo- Geita

Waumini ya dini ya kiislam mkoani Geita wamekumbushwa matumizi sahihi ya utumiaji wa virutubisho tiba ili kujikinga na maradhi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Dkt. Khalid Hussein kutoka taasisi ya utafiti na ugunduzi ya TABCCOM Herbal Research Center and Rescue Community Wellbeing Tanzania ya Dar es salaam ambaye ni mgunduzi wa virutubisho vya asili vya Kasi Mix vinavyoimarisha na kuongeza kinga ya mwili (CD4), kutibu malaria, kuondoa uchovu na kuongeza nguvu za mwili pamoja na kuondoa msongo wa mawazo.

Sauti ya Dr. Khalid Hussein kutoka taasisi ya Utafiti na Ugunduzi ya TABCCOM herbal research center and rescue community wellbeing Tanzania akiwa Geita na kuzungumzia umuhimu wa Lishe bora.