Storm FM

Wafanyakizi Storm FM wafika bungeni Dodoma

22 June 2023, 12:53 pm

Na Mrisho Sadick: Baadhi ya Wafanyakazi wa Storm FM Redio (Sauti ya Geita) leo Juni 22,2023 wametembelea Bungeni Jijini Dodoma kushuhudia uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibunge kwa mwaliko wa Mbubge wa Jimbo la Geita mjini Mhe Constantine Kanyasu.

Wafanyakazi hao ni Ester Mabula , Said Sindo watangazaji wa kipindi Cha Storm Asubuhi na Meneja wa Kituo Cha Storm FM Obadia Mashamba pamoja na mambo mengine wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Geita kwa mwaliko huo.