Storm FM

Jeshi la zimamoto Geita latoa elimu kwa wanafunzi

28 April 2026, 7:07 pm

Afisa wa Jeshi la zimamoto akitoa maelekezo ya namna ya kuzima moto kwa kutumia maji. Picha na Ester Mabula

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita limetoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi kuelekea siku ya wazima moto Duniani ambayo huadhimishwa kila Mei 04 ya kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka mashujaa waliopotea maisha katika shughuli za uokoaji.

Na: Ester Mabula

Elimu ya kukabiliana na majanga ya moto imetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi Mseto na Bombambili zilizopo katika halmashauri ya manispaa ya Geita.

Akizungumza Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Mrakibu msaidizi Keneth Mwakasitu amesema lengo la kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya msingi ni kuhakikisha elimu inawafikia Jamii kuanzia umri wa utotoni

Sauti ya Kaimu Kamanda wa Zimamoto Kenneth Mwakasitu
Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mrakibu msaidizi Kenneth Mwakasitu. Picha na Ester Mabula

Walimu wa shule hizo Mwl. Japhet Msilanga na Mwl. Mwanaisha Hamza wametoa pongezi kwa Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wakieleza itasaidia kuwajengea uelewa zaidi hata katika masomo yao.

Sauti ya walimu wa shule za Mseto na Bombambili
Wanafunzi wa shule ya msingi Mseto wakifurahia burudani baada ya kupewa elimu. Picha na Ester Mabula

Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa elimu wamesema watatumia elimu hiyo kuwaelimisha wengine sambamba na kuwakumbusha wazazi kupiga namba ya msaada pindi majanga yanapojitokeza.

Sauti ya wanafunzi wa shule za Mseto na Bombambili

Jeshi la zimamoto na uokoaji nchini limeendelea kufikisha elimu kwenye Jamii kwa kuyafikia makundi mbalimbali ambapo Balozi wa zimamoto Mwalimu Yusuph Ibrahim  amesema Jamii imeendelea kupata uelewa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.

Sauti ya Balozi wa zimamoto Mwl. Yusuph Ibrahim
Wanafunzi wa shule ya Bombambili English Medium School wakisikiliza maelekezo ya maafisa wa zimamoto. Picha na Ester Mabula