Storm FM

Wafanyabiashara wa samaki walia na ushuru njiani, Geita

2 January 2024, 8:41 am

Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Joshoni, Nyankumbu, Geita. Picha na Zubeda Handrish

Kilio kimeendelea kwa wafanyabiashara wa samaki kutozwa tozo kubwa wanawapokuwa njiani wakati wanataka kuzifikisha samaki hizo sokoni na kuamua kutoa ya moyoni.

Na Zubeda Handrish- Geita

Wafanyabiashara wa samaki katika soko la jioni (Joshoni) Nyankumbu mjini Geita, wamezungumzia changamoto ya usafirishaji wa samaki kutoka kwenye miyalo hadi sokoni.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Storm FM sokoni hapo na kusema kuwa tozo njiani zimekuwa kubwa ukilinganisha na mzigo aliochukua wa samaki.

Sauti ya wafanyabiashara wa samaki katika soko la Joshoni, Nyankumbu, Geita

Kufuatia malalamiko hayo Storm FM imezungumza na Afisa Uvuvi wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Makoye Kafuku kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko hayo, ikiwemo ya kutozwa ushuru kwa kila kichwa cha samaki, pamoja na utaratibu wa halmashauri katika tozo hizo.

Sauiti ya Afisa Uvuvi wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Makoye Kafuku

Aidha amesema tozo hizo zinategemea na halmashauri husika samaki hizo zilipochukuliwa, na halmashauri ulizopitisha samaki kabla ya kufika halmashauri ya mji wa Geita na kufikishwa sokoni.

Sauiti ya Afisa Uvuvi wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Makoye Kafuku