Storm FM

GGML yafadhili vipimo bure kwa wananchi kupitia ICAP

10 October 2024, 10:41 am

Jackson Joston, Afisa msimamizi wa upimaji kutoka ICap akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Kampuni ya Geita Gold Minning Limited inayojihusisha na uchimbaji madini ya dahabu mkoani Geita imeendelea kurejesha kwa jamii kupitia utoaji na uwezeshaji wa huduma mbalimbali zinazowalenga wananchi.

Na: Ester Mabula – Geita

Kampuni ya GGML ikishirikiana na shirika la ICAP imeendelea kutoa huduma za vipimo na matibabu bure kwa wananchi wa mkoani Geita katika maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA mjini Geita.

Jackson Joston, Afisa msimamizi wa upimaji kutoka ICap, amesema wamepokea zaidi ya watu 300 ambapo watatu tu waligundulika na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wengine wakigundulika kuwa na maambukizi ya maradhi mengine.

Sauti ya Jackson Joston

Neema Lubaga ni meneja mtekelezaji wa ICAP ameeleza namna wanavyotoa huduma za afya kwa jamii kupitia vipimo vya magonjwa mbalimbali

Sauti ya Neema Lugaba
Neema Lugaba, Meneja mtekelezaji wa shirika la ICAP akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Salim Awadhi ni dereva na msimamizi wa gari ambalo linahusika kutoa huduma ya vipimo, anaeleza namna wanavyotumia gari hilo kufikisha huduma kwa jamii.

Sauti ya Salim Awadhi
Samweli Kayola, mmoja ya wananchi waliojitokeza kwaajili ya kufanya vipimo. Picha na Ester Mabula

Baadhi ya wanufaika wa mpango huu ambao ni wananchi wameeleza kuridhishwa na hatua za GGML kuendelea kuikumbuka jamii kwa kushirikiana na ICap wakisema imewasaidia kujua hali ya afya zao.

Sauti ya wananchi

Vipimo vinavyotolewa ni pamoja na tezi dume, sukari, presha, saratani ya kizazi, na virusi vya UKIMWI.

Gari linalotoa huduma za vipimo ambalo linatembea maeneo mbalimbali kuwafikia wananchi. Picha na Ester Mabula

Mpango huu ni mikakati ya GGML kuendelea kuikumbuka Jamii na kurejesha kwa Jamii ili kuchochea ustawi wa afya bora na maendeleo kwa ujumla.