Storm FM

Mashabiki wa soka Geita wafunguka baada ya raundi 2 ligi kuu bara

1 September 2023, 5:31 pm

Shabiki wa soka mtaa wa Nyankumbu, Geita akifunguka juu ya ligi kuu. Picha na Zubeda Handrish

Mengi yamejiri tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi, huku kila timu ikitaka kujichukulia pointi zake mapema.

Na Zubeda Handrish- Geita

Mashabiki wa soka kutoka mtaa wa Nyankumbu, Kata ya Nyankumbu, wilayani na mkoa wa Geita, wamefunguka juu ya hali ya Ligi Kuu ya NBC kwa sasa ikiwa ni raundi 2 tu tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2023/24 Agosti 15.

Wamesema Ligi imeanza kwa kuchangamka na ushindani wa hali ya juu hivyo matarajio ni makubwa kwa mashabiki na vilabu vyao.

Sauti za Mashabiki wa soka mkoa wa Geita wakifunguka juu ya hali ya Ligi Kuu ya NBC kwa sasa