Storm FM

Atelekezwa baada ya kubeba ujauzito Geita

4 May 2021, 6:47 pm

Na Mrisho Sadick:

Msichana (15) Mkazi wa Mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita ametelekezwa na mume wake alieahidi kumuoa baada ya kubeda ujauzito.

LETISIA MASANJA

Msichana huyo anaefahamika kwa jina la Letisia Masanja  mzaliwa wa wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ambae alipotezana na wazazi wake wakati akiwa Mdogo nakukumbilia Geita amesema mwanaume huyo alimdanganya kuwa ataishi nae nakumtorosha alipokuwa akiishi na alipo beba ujauzito akafukuzwa.

Letisia Masanja

Letisia Masanja akiwa na rafiki yake Mkono wa kushoto Rose Marwa

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa 14 Kambarage Maulid Mrisho amesema serikali ya mtaa huo imeendelea na jitihada za kumtafuta mwanaume huyo ili kunusuru maisha ya mtoto pamoja na mama yeke kwani kwasasa hawana mahala pa kuishi.

Mwenyekiti Maulid Mrisho