Storm FM

Utalii wa ndani umeongezeka kwa 159%

4 December 2023, 1:50 pm

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdidit Katwale akiwa na Waziri wa Madini Antony Mavunde. Picha na Mrisho Sadick

Elimu ya utalii imeendelea kuwaingia wananchi hali ambayo imekuwa ikichochea ukuaji wa utalii wa ndani kwa kasi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Idadi ya utalii wa ndani imeongezeka kwa asilimia 159 mwaka 2023 huku wananchi wakihimizwa kuendelea kutembelea nakuwekeza kwenye vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini ili kukuza pato la taifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa madini Antony Mavunde kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko wakati akifunga rasmi tamasha la Chato Utalii Festival ambapo amesema idadi ya watalii wa ndani mwaka 2021 ilikuwa ni zaidi ya laki saba huku mwaka 2023 ikiwa ni zaidi ya milioni mbili sawa na ongezeko la asilimia 159%.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa Mkoa wa Geita Cornel Magembe amewataka wananchi wa chato na Geita kutumia fursa ya tamasha hilo kujenga mahusiano ya kibiashara na wageni waliofika kutoka maeneo mbalimbali kwa kuwekeza kwenye sekta ya utalii.

Sauti ya Waziri mavunde na kaimu RC Geita
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya ufungaji wa tamasha la Chato Utalii Festival

Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandis Deusdedit Katwale amesema wataendelea kutumia rasilimali zilizopo katika wilaya hiyo kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Chato

Katika kuiunga mkono serikali Benki ya NMB ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa Tamasha hilo imetoa madawati 200 na mabati 150 katika shule 5 za msingi na sekondari  huku Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi mjini Geita Frank Changawa akibainisha mikakati ya usambazaji maji wilayani chato.