Storm FM

Ugonjwa wa ajabu wamtesa Fikiri anaomba msaada wa Matibabu

22 June 2023, 8:29 am

Fikiri Manyilizu Mkazi wa Muleba Kagera

Na Zubeda Handrish: Fikiri Manyilizu mwenye umri wa miaka (31) Mkazi wa Muleba Mkoani Kagera amemuomba Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu msaada wa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu ambao umemsumbua kwa muda mrefu.

Fikiri anasema katika familia yake wamebaki wawili yeye pamoja na kaka yake na ugonjwa huo wa ajabu ulianza akiwa na umri wa miaka saba baada ya wazazi wake kufariki dunia na amezunguka katika Hosptali mbalimbali kutafuta matibabu bila mafakio.

Akiwa katika harakati za kupambania uhai wake Fikiri alifika katika Hosptali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza wataalaamu wa afya katika eneo hilo walimshauri aende Hosptali ya taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi ya juu ugonjwa huo , kikwazo katika hilo ni fedha ya kumfikisha huko , nakuamua kumuangukia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na watanzania.

Fikiri Manyilizu Mkazi wa Muleba Kagera

Akiwa Mkoani Geita katika harakati za kuomba fedha ya matibabu Firiki amesema kwa yoyote ambae ataguswa kumsaidia atumie namba yake ya mawasiliano ambayo ni 0754255354.