Storm FM

Storm FM funga mwaka

17 December 2022, 2:13 pm

Na Zubeda Handrish:

Storm FM tukiwa tunaukamilisha mwaka 2022 tunafunga na Bonanza la Funga Mwaka kwa kushirikisha vilabu vya soka na michezo mbalimbali siku ya kufunga.

Leo Dec 17, 2022 ni ufunguzi wa bonanza hilo ambapo zinaanza timu za Shadow Gin na Kifaru FC katika mchezo wa ufunguzi katika viwanja vya shule ya Sekondari Kalangalala majira ya saa 9:00 alasiri shughuli zitaanza huku mgeni rasmi wa ufunguzi huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Geita, Ally Twisti.