Storm FM

Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya Vyatakiwa Kuhakiki Vipimo

20 May 2021, 7:51 pm

Na Mrisho Sadick:

Hospitali za wilaya na vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoani Geita zimetakiwa kufanya uhakiki wa vipimo ili kuondoa utata katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa wakala wa Vipimo Mkoani Geita Bw Moses ezekieli katika Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Geita wakati akifanya uhakiki wa vipimo.

Aidha Bw Moses amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuhakiki mizani kwa maana kuna muepusha mgonjwa kupata madhara ya afya anapotumia dozi.
Baadhi ya maafisa wa vipimo Mkoani Geita wamesema uhakiki wa vipimo ni endelevu nakwamba kila kipimo angalau kihakikiwe mara moja ndani ya kipindi cha miezi 12 au pale mtumiaji ama mnunuzi atakapokuwa na wasiwasi na kile anachokipata kwenye kipimo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Geita Dkt Paschal Mjuni amesema wamekuwa wakifanya zoezi la kuhakiki vipimo mara kwa mara kwasababu vikiwa sahihi na huduma pia zinaweza kuwa sahihi.
Kila Mei 20 ya kila mwaka huadhimishwa siku ya vipimo dunia na kaulimbiu ya mwaka huu niĀ  Afya kwa Vipimo.