Storm FM

Wakumbwa na mshangao kijana kufariki kwa kuchomwa kisu

23 July 2023, 2:30 pm

Wananchi wa Muembeni katika tukio la kifo. Picha na Zubeda Handrish

Matukio ya kiuhalifu na kujichukulia sheria mkononi yamekithiri katika baadhi ya mitaa mkoani Geita, jambo linalosababisha baadhi ya vifo kutokea, huku wananchi wakishindwa kutoa taarifa katika vyombo husika juu ya uhalifu huo.

Na Zubeda Handrish- Geita

Katika hali ya kusikitisha kijana anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22-23 aliyefahamika kwa jina moja maarufu la Matikiti amefariki dunia kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu, ambapo bado hawajafahamika na baada ya kutekeleza tukio hilo walitokomea kusikojulikana.

Wananchi wa Muembeni katika tukio la kifo. Picha na Zubeda Handrish

kufuatia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamesimulia kwa kina kuhusi kifo cha kijana huyo.

Sauti ya Wananchi wa Muembeni kuhusu tukio la kifo

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Mwembeni Manyema Mathias amesema kijkana huyo alikuwa amejiunga katika makundi mabaya hivyo akawaomba wazazi kusimami katika malezi ya watoto wao.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Mwembeni Manyema Mathias

Nae Mkuu wa upelelezi wilaya ya Geita Rashid Maganyilo akiwa katika mkutano wa wananchi ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Geita mjini Mhe. Costantine Kanyasu, amesema tukio hilo amelipata na alifika eneo la tukio.

Sauti ya Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Geita Rashid Maganyilo

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mtandao wa BBC inaeleza kuwa  asilimia 14 ya matukio ya mauaji nchini yanasababishwa na ugomvi na hasira hivyo inaaswa kutojichukulia sheria mkononi.