Storm FM

Wanafunzi wasifu ujenzi wa shule Mpya Geita

19 April 2021, 6:34 pm

Wanafunzi Wa Shule Ya Sekondari Ya Evarist Iliyopo Kata Ya Nyarugusu Wilayani Geita Wameipongeza Serikali Kwa Kushirikiana Na Wadau Wa Maendeleo Katika Eneo Hilo Kwa Kufanikisha Ujenzi Wa Shule Hiyo.

Wakizungumza Katika Shule Hiyo Ambayo Imeanza Kutoa Elimu Ya  Kidato Cha Kwanza, Wamesema Imesaidia Kupunguza Changamoto Za Kutembea Umbali Mrefu Pamoja Na Mrundikano Wa Wanafunzi Katika Shule Kongwe Ya Sekondari Ya Nyarugusu.

Wanafunzi

Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Nyarugusu Bw Mussa Kiote Amesema Shule Hiyo Imepewa Jina La Evarist Ambae Ni Mkurugenzi Wa Mgodi Wa STAMICO Kwa Kutambua Mchango Wake Katika Ujenzi Huo Nakusema Kuwa Shule Hiyo Itasaidia Kupunguza Changamoto Nyingi Kwa Wanafunzi.

Shule Hiyo Imejengwa Na Serikali Kwa Kushirikiana Na Wadau Mbalimbali Wa Maendeleo  Wakiwemo Wachimbaji Wadogo Wa Madini Ya Dhahabu  Wa Mgodi Wa Stamico Na Imeanza Na Idadi Ya Wanafunzi 300 Wa Kidato Cha Kwanza.