Storm FM

Wakazi wa Mtaa wa Ujamaa Geita walalamikia kero ya Uchafu machinjioni

19 April 2021, 5:55 pm

Na Kale Chongela:

Wakazi Wa Mtaa wa Ujamaa Kata ya Kalangalala Halmashauri ya Mji Wa Geita Wameuomba Uongozi wa Eneo Hilo Kutatua Chagangamoto ya Uchafu Katika Eneo La Machinjioni.

Wakizungumza na Storm FM Wananchi Wa Mtaa Huo Wamesema Hali hiyo imekuwa Changamoto Kubwa Kwa Muda Mrefu na Kuuomba uongozi wa serikali ya Mtaa wa Ujamaa Kutatua Changaoto hiyo kwani inaweza Ikasababisha Mlipuko ma Maradhi.

Wakazi wa Ujamaa

Aidha Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa  Huo Bw Musa Baruku Amekiri Kuwepo Kwa Hali Hiyo  Mara Baada Ya Kupokea Malalamiko  Kutoka Kwa Wananachi Wakati Ambapo Serikali Ya Mtaa Wakisubiri Kupata Suluhu Ya Changamoto Hiyo .

Naye Diwani Wa Kata Ya Kalangalala Bw Prudence Temba  Amesema Mikakati Ya Uongozi Wa Kata Kwa Sasa Ni Kuhamisha Machinjio Hayo  Ili Kuhamia Machinjio Ya Kisasa Yaliyopo Mtaa Wa Mpomvu.