Storm FM

Shamba la migomba lafyekwa Geita.

3 August 2021, 2:26 pm

Na Zubeda Handrish:

Shamba la migomba lenye ukubwa wa ekari mbili limeharibiwa na watu wasiojulikana ikisemekana kuwa chanzo cha uharibifu huo ni mgogoro wa Ukoo dhidi ya Shamba hilo.

Mmiliki wa Migomba hiyo Bw. Faida Lunsalia amesikitishwa na kitendo hicho nakudai kuwa hata kama ameshindwa kesi ya umiliki wa Shamba hilo hakukuwa na sababu ya kukatiwa Migomba yake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo amesema hajapokea kesi yoyote kuhusu uharibifu wa Migomba nakwamba ataendelea kufuatilia.