Storm FM

Ubovu wa barabara wakwamisha maendeleo

12 March 2024, 3:05 pm

Baadhi ya sehemu ya Barabara ya kutoka stendi hadi soko la Mbagala zilizoharibika vibaya. Picha na Mrisho Sadick

Kuharibika kwa miundombinu ya barabara nakutelekezwa kwa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo imekuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wengi

Na Mrisho Sadick – Geita

Wakazi wa mitaa ya Katundu na Moringe Halmashauri ya Mji wa Geita wameiomba serikali kuijenga kwa kiwango cha lami barabara inayotoka stendi kuu ya mabasi hadi soko  la Mbagala kwani inawapa changamoto wakati wa usafirishaji wa mizigo kuingia kwenye soko hilo.

Wakizugumzia changamoto ya Barabara hiyo yenye urefu wa mita 900 ambayo kwa kiasi kikubwa inatumiwa na wafanyabiashara wa soko la mbagala pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kalangalala na Kisesa wamesema nyakati za mvua hali inakuwa mbaya.

Sauti ya Wananchi

Wafanyabiashara wa soko hilo wanasema mvua inaponyesha maji huingia kwenye Biashara zao na kuwasababishia hasara kubwa.

Baadhi ya sehemu ya Barabara ya kutoka stendi hadi soko la Mbagala zilizoharibika vibaya. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Wafanyabiashara

Akizungumza na Channel Ten Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Ezila Daniel amesema tayari wameshampata mkandarasi mpya na barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.

Sauti ya Meneja TANROAD Mkoa wa Geita