Storm FM

Polisi kata hewa wachukuliwe hatua

19 July 2023, 10:33 am

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo. Picha na Said Sindo

Matukio ya uhalifu yakiwemo ya wizi na udokozi yameendelea kuwa changamoto katika baadhi ya mitaa na vijiji, jambo lililopelekea Kamanda Jongo kuwataka Polisi kata kuwajibika ipasavyo.

Na Said Sindo- Geita

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo amewaagiza madiwani kumpa taarifa endapo kuna kata ambayo polisi kata wake ni hewa na hawatekelezi majukumu yao.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo

Amesema ni lazima kila kata iwe na polisi kata anayesimamia kikamilifu suala la ulinzi na usalama kwa kushirkiana na viongozi wa kata ili kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi na polisi jamii.