Storm FM

Wanafunzi kidato cha nne wapewe nafasi na uhuru wakati wote wa mtihani

13 November 2023, 11:41 am

Wanafunzi wa shule ya sekondari Katoro na Ludete wakiwa katika kongamano la kupinga vitendo vya ukatili. Picha na Mrisho Sadick.

Kuanza kwa mtihani wa kidato cha nne kumeisukuma taasisi ya mtetezi wa mama wilayani Geita kuandaa kongamano la kuwaombea nakuwapatia vifaa watahiniwa katika shule za Katoro na Ludete.

Na Mrisho Sadick:

Wazazi na walezi Mkoani Geita wametakiwa kuwatimizia mahitaji ya msingi nakuwapunguzia majukumu wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuanza mtihani wa Taifa Novemba 13 mwaka huu ili kuwapa nafasi ya kujiandaa vizuri.

Viongozi wa taasisi ya mtetezi wa mama na wadau wa kupinga ukatili wakiwa katika shule ya sekondari Katoro. Picha na Mrisho Sadick

Rai hiyo imetolewa na viongozi wa dini na wakuu wa Shule za Sekondari Katoro na Ludete wilayani Geita katika kongamano la kuwaombea nakuwapatia vifaa mbalimbali wanafunzi wa kidato cha nne lililoandaliwa na taasisi ya Mtetezi wa mama  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu Mkoani Geita.

Sauti ya kiongozi wa dini na Mwalimu

Mwenyekiti wa taasisi ya mtetezi wa mama wilaya ya Geita Elizabeth Coster amesema sambamba na Kongamano hilo Taasisi hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo huku kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo akisema vitendo vya uaktili ikiwemo ubakaji vimeendelea kupungua.

Sauti ya Mwenyekiti na Kamanda wa Polisi Geita