Storm FM

Waziri Jafo aipongeza GGML kwa kuendelea kutunza mazingira

26 September 2023, 7:05 pm

Waziri Selemani Jafo katika maonesho ya 6 ya kimataifa ya teknolojia ya madini. Picha na Kale Chongela

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na meneja wa TFS miti 400 imepandwa katika viwanja vya EPZA Bombambili na Mhe. Jafo.

Na Kale Chongela- Geita

Waziri Wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingiara Mhe. Selemani Jafo ameipongeza GGML Kwa kuendelea kutunza mazingira kwa kiwango kikubwa .

Mhe. Jafo amesema hayo akiwa katika uwanja Wa EPZ ambapo ndipo yalipo maonesho ya sita ya kimataifa ya Madini mjini Geita.

Waziri Wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingiara Mhe. Selemani Jafo

Akiwa katika banda la GGML amesema Mgodi huo umekuwa chachu kubwa katika suala la utunzaji wa mazingira huku akisisitiza wananchi kupanda miti.