Storm FM
Storm FM
2 August 2026, 7:01 pm

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mgusu wakitumia kompyuta walizokabidhiwa. Picha na Kale Chongela
Kompyuta hizo zitawasaidia wanafunzi kupata ujuzi wa matumizi ya TEHAMA na kuongeza uwezo wao wa kujifunza kwa njia za kisasa.
Na: Kale Chongela
Diwani wa Kata ya Mgusu Manispaa ya Geita Yohana Yusuph Buhabi amekabidhi kompyuta 43 kwa Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Diwani Buhabi amesema vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi kupata ujuzi wa matumizi ya TEHAMA na kuongeza uwezo wao wa kujifunza kwa njia za kisasa.
Sauti ya Diwani wa Kata ya Mgusu Manispaa ya Geita
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mgusu, Mwalimu Sancho Ruguga, ameishukuru Ofisi ya Diwani kwa msaada huo, akisema kompyuta hizo zitachangia kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Kwa upande wake, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyesoma risala ya shukrani amesema ujio wa kompyuta hizo utawasaidia wanafunzi kupata maarifa ya TEHAMA na kujifunza kwa ufanisi zaidi ili kuendana na maendeleo ya teknolojia.
Sauti ya mwanafunzi aliyesoma risala ya shukrani
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Chacha Wambura, Katibu wa Mbunge huyo, Riziki Marko amesema kompyuta hizo ni mchango muhimu katika kuinua kiwango cha elimu na kuwajengea wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Miyenzi ameuagiza uongozi wa Shule ya Sekondari Mgusu kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa kwa uangalifu ili viweze kudumu na kuwanufaisha wanafunzi wa sasa na vizazi vijavyo.
Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita

Picha ya pamoja viongozi waliofanikiwa kuhudhuria makabidhiano hayo akiwemo Diwani Buhabi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Miyenzi. Picha na Kale Chongela