Storm FM

Mbunge Chacha atatua changamoto ya umeme na maji zahanati ya Mwatulole

22 August 2026, 12:14 am

Muonekano wa Jengo la zahanati ya Mwatulole lililopo kata ya Buhalahala manispaa ya Geita. Picha na Ester Mabula

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura ameendelea kutatua changamoto za waananchi katika jimbo lake kwa kufanya ziara katika maeneo mbalimbali sambamba na kusikiliza kero za wananchi.

Na: Ester Mabula

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura mapema jana Agosti 21, 2026 ametembelea zahanati ya Mwatulole iliyopo katika kata ya Buhalahala manispaa ya Geita kwa lengo la kuona utoaji wa huduma za kiafya sambamba na kutatua changamoto zilizopo katika zahanati hiyo.

Akizungumza na watumishi wa zahanati hiyo sambamba na wananchi wa eneo hilo amesema kuwa dhamira yake kuu ni kutatua changamoto za wananchi ambapo ameahidi kusogeza huduma ya umeme katika zahanati hiyo pamoja na kuwezesha upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Sauti ya mbunge mhandisi Chacha Wambura
Mbunge wa jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

David Yusuph ni Muuguzi mkunga katika zahanati hiyo amesema zahanati hiyo inahudumia jumla ya wagonjwa 200 kwa mwezi ambapo upatikanaji wa umeme utasaidia baadhi ya huduma kutolewa kwa urahisi.

Sauti ya David Yusuph, muuguzi zahanati ya Mwatulole
David Yusuph, muuguzi zahanati ya Mwatulole akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole Bw.  Edward Misalaba pamoja na wananchi wa eneo hilo akiwemo Bw, Cassian Mtesigwa na Bi. Lucy Zacharia wamempongeza mbunge kwa hatua hiyo na kueleza kuwa itasaidia na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi.

Sauti ya mwenyekiti na wananchi