Shule ya sekondari Bugalama wapanda miti 500 kutunza mazingira
28 November 2024, 10:30 am
Serikali na wadau mbalimbali wa mazingira wameendelea kuhamasisha jamii juu ya upandaji miti ambapo kwa mujibu wa wataalam wanaeleza kuwa miti imekuwa na faida nyingi katika kutunza mazingira.
Na: Kale Chongela – Geita
Uongozi wa shule ya sekondari Bugalama iliyopo kata ya Bugalama halmashauri ya wilaya ya Geita wamepanda miti 500 kwaajili ya matunda, kivuli ikiwa ni jitihada za kuendelea kutunza mazingira.
Akizungumza na Storm FM Novemba 26, 2024 akiwa shuleni hapa mkuu wa shule hiyo Mwl. Gibson Mkomi amesema lengo la kupanda miti hiyo ni kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira ya shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waeleza kuwa jukumu kubwa ni kuendelea kutunza mazingira ya shule kwa kupanda miti ambayo itasaidia kuondokana na changamoto ya uharibifu wa mazingira.
Diwani wa viti maalumu halmashauri ya wilaya ya Geita Bi. Veronica Migelegele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo amewasihi wananchi kujenga desturi ya kupanda miti.