Storm FM

TWCC yatoa elimu kwa wajasiriamali Geita

19 June 2024, 4:23 pm

Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo ya TWCC. Picha na Kale Chongela

Chemba ya wanawake wafanyabiashara mkoa wa Geita (TWCC) imetoa elimu katika mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali halmashauri ya mji wa Geita juu ya uboreshaji wa bidhaa.

Na: Kale Chongela – Geita

Serikali mkoani Geita imewataka wajasirimali kuendelea kujenga desturi ya kujadili kwa pamoja na kubaini changamoto ambazo zinawakabili ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza na wajasiriamali Juni 18, 2024 mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali yaliyoandaliwa na chemba ya wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Aloysius, amebainisha kuwa ipo haja kwa wajasiriamali kujiwekea utaratibu wa kukutana ili kujadili mafanikio na changamoto zao.

Sauti ya RC Geita
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na wajasiriamali (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Rais wa TWCC nchini Tanzania Bi. Mercy Sila ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujitokeza katika soko huru la Afrika ili kuendelea kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara mbalimbali.

Sauti ya Mercy Sila
Mkuu wa mkoa wa Geita (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa TWCC na SIDO. Picha na Kale Chongela

Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali waliopatiwa mafunzo hayo Bi. Halima Chembemoyo amepongeza na kushukuru kwa hatua hiyo.

Sauti ya mjasiriamali

Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO mkoa wa Geita Bi. Nina Nchimbi ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wajasiriamali ili waweze kufikia mafanikio yao.

Sauti ya meneja SIDO