Storm FM

Waandishi wa habari Geita waanzisha mradi

20 July 2023, 2:20 pm

Mwenyekiti wa GPC Renatus Masuguliko akikabidhi Pikipiki. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya ametoa wito kwa klabu zingine nchini kuiga uanzishaji wa miradi ya kujiingizia kipato kama klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita kwa kuanzisha mradi wa pikipiki.

Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa juma lililopita wakati akishuhudia makabidhino ya pikipiki kwa ajili ya kukodishwa na kuingiza kipato katika klabu hiyo ambapo pikipiki hiyo iliyonunuliwa na GPC ina thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano 2,500,000.

Simbaya amesema kuwa GPC imeanza kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya UTPC “FROM GOOD TO GREAT” ambapo klabu zimetakiwa kupunguza utegemezi kutoka kwa wahisani hasa vitu vidogo ambavyo klabu inaweza kufanya kujipatia kipato.

Sauti ya Mkurugenzi wa (UTPC) Kenneth Simbaya
Mkurugenzi wa (UTPC) Kenneth Simbaya aliye katikati akizungumzia mradi huo wa Pikipiki. Picha Mrisho Sadick

Walioshuhudia hafla hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa GPC Renatus Masuguliko,Katibu wa GPC Novatus Lyaruu ,Mweka hazina wa GPC Editha Edward, Salum Maige na miongoni mwa wengine.