Storm FM

Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ashambuliwa kwa panga Katoro

7 May 2024, 5:03 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) . Picha na Kale Chongela

Matukio ya watu wenye ulemavu wa ngozi kushambuliwa yalilitia doa taifa la Tanzania miaka ya nyuma, dalili za vitendo hivyo kuanza tena imeleta taharuki.

Na Kale Chongela – Geita

Mtoto wa miaka 10 mwenye ulemavu wa ngozi mkazi wa mtaa wa Mtakuja kata ya Katoro wilayani Geita amejeruhiwa kwa panga na mtu asiyejulikana na kuzua taharuki.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishna Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo ni la kupangwa.

Kamanda Jongo amesema kuwa majeraha ya mtoto na silaha iliyokutwa eneo la tukio ni wazi aliyefanya tukio hilo hakuwa na lengo la kuondoka na kiungo chochote.

Sauti ya kamanda wa Polisi Geita

Mganga mfawidhi wa hospital ya mji wa Geita Thomas Mafuru amethibitisha kumpokea mtoto huyo ambae alikuwa amejeruhiwa kichwani na mkononi nakwamba anaendelea vizuri.

Sauti ya Mganga Mfawidhi

Kwa upande wake  mama mzazi wa mtoto huyo na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wamesema wamelipatwa na hofu juu ya tukio hilo.

Sauti ya mama wa mtoto