Storm FM

Afariki dunia baada ya kusombwa na maji akivuka mto

29 December 2022, 7:55 pm

Na Mrisho Sadick :

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Benjamini John mwenye umri wa miaka (30) Mkazi wa Kata ya Kasamwa Halmashauri ya mji wa Geita amefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akijaribu kuvuka kwenye mto kwenda upande wa pili.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita  Inspekta Edward Lukuba amethibitisha kutokea  kwa tukio hilo, huku chanzo chake kikitajwa kuwa nikuongezeka kwa maji katika Mto Nyampa Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwasasa, huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari katika kipiki hiki cha mvua.

.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyampa lilipotokea tukio hilo Bi, Herena Maneno  amesema, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wake kuwa wameona mwili wa mtu ukiwa unaelea katika Mto, ndipo alipotoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa huo wameiomba serikali kuwajengea daraja katika eneo hilo ili kuepukana na matukio ya watu kufa maji kwakuwa eneo hilo linatumiwa na watu wengi hususani wakulima.

.