Storm FM

Wananchi washirikiana kuziba chanzo cha mafuriko

13 April 2024, 2:35 am

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mbugani waliojitokeza kutengeneza eneo korofi la mtaro lililosababisha nafuriko mtaani hapo. Picha na Kale Chongela

Uduni wa miundombinu ya barabara imekuwa ikichangia athari mbalimbali ambazo zimekuwa zikisababishwa na mvua inayoendelea kunyesha mkoani Geita

Na Kale Chongela – Geita

Baada ya mafuriko kuikumba mitaa mbalimbali ya mkoa geita kutokana na mvua iliyonyesha siku ya April 7, 2024 na kusababisha changamoto kwa wakazi wa mtaa wa Mbugani kata ya kalangalala halmashauri ya mji wa geita.

Hali hiyo imewalazimu baadhi ya wakazi wa mtaa huo wa Mbugani kushirikiana kwa pamoja kuziba eneo ambalo lilikuwa linapitisha maji kutoka katika mtaro unaopitisha maji katika eneo hilo, mtaro uliopasuka kutokana na kuelemewa na maji hivyo kusababisha athari hiyo.

Miongoni mwa wakazi wa mbugani waliojitokeza kurekebisha eneo korofi la mtaro. Picha na kale Chongela

Wananchi hao wakiwa eneo hilo wamebainisha kuwa mtaro huo umekuwa ukipitisha maji ambayo yanatirirrika wakati mvua ikinyesha hali ambayo imekuwa ikipelekea maji kutapakaa kwenye makazi ya watu wa eneo hilo.

Sauti za baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mbugani

Kwa upande wake Diwani wa kata ya kalangalala Bw. Prudence Temba ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kujitolea huku akiwataka wananchi wengine wa kata hiyo kujitolea kwenye shughuli za kijamii.

Sauti ya diwani kata ya Kalangalala