Storm FM

Ajinyonga hadi kufa kisa kakutwa na vvu Geita.

3 May 2021, 6:18 pm

Na Mrisho Sadick:

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Henry Mwaibambe amethibitisha tukio la Shija Mwanzalima (30) Mkazi wa Mtaa wa Nyantorotoro A mjini Geita kujinyonga hadi kufa.

Kamanda amesema kabla ya Shija kufanya kitendo hicho alimjeruhi Mtoto wake wa kambo tumboni kisha yeye kujinyonga hadi kufa huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni kugundua kuwa ana maambukizi ya virus vya Ukimwi.

RPC Geita

Mtoto huyo alijeruhiwa kwa kuchanwa na kitu chenye ncha kali tummboni, alifikishwa katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Geita kwa ajili ya kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri.