Storm FM

Wajitolea kuwasaidia wazee wasiojiweza

26 July 2023, 10:37 pm

Moja ya mzee aliyesaidiwa. Picha na Kale Chongela

Kusaidia ni moyo na si utajiri kama msemo wa wahenga, hivyo unaweza kusaidia pale penye uhitaji kama ambavyo amesisitiza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magogo B.

Na Kale Chongela- Geita

Jamii imekumbushwa kujenga desturi ya kuwatembelea wazee na kuwasaidia kwa kidogo walichonacho ili waweze kuepukana na changamoto ambazo zinawakumba.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magogo B kata ya Buhalahala mjini Geita, Bw. Juma Ramadhani baada ya kutoa msaada kwa baadhi ya wazee waliopo katika eneo hilo ambapo amesema ni vyema kila mmoja kutumia kidogo alichonazo kwa kuwasaidia wazee wasiojiweza.

Sauti ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magogo B

Aidha baadhi ya wananchi ambao wameshiriki katika kutoa msaada huo wametumia fursa hiyo kwa kuwataka vijana kuhakikisha wanawasaidia wazee wao na si kuwatelekeza jambo ambalo linaibua sintofahamu katika jamii.

Sauti ya wananchi wa Magogo B