Storm FM

Wananchi wampongeza mwenyekiti kwa kutatua kero zao

12 September 2023, 1:23 pm

Takribani wiki moja imepita tangu Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Geita kuwaagiza wenye viti wa mitaa/vijiji pamoja na watendaji kuhakikisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu, huku ikiwa ni kawaida kwa mtaa wa Shilabela.

Na Said Sindo- Geita

Wananchi katika mtaa wa Shilabela, kata ya Buhalahala,  mjini Geita wameishukuru na kuipongeza Serikali ya mtaa huo kwa kuwashirikisha katika miradi inayotekelezwa na Serikali na kutatua kero na changamoto zao.

Wamesema ushirikishwaji huo unawafanya kutambua matumizi ya mapato yanayokusanywa na mtaa wao kwa maendeleo ya mtaa huo huku wakisema mwenyekiti wao amekuwa mstari wa mbele kuwaletea maendeleo.

Sauti ya wananchi wa mtaa wa Shilabela
Sauti ya wananchi wa mtaa wa Shilabela

Akizungumza na Storm FM ofisini kwake, Mwenyekiti wa mtaa huo Fredrick Masalu amesema ni utaratibu wa serikali ya mtaa huo kuwasomea wananchi mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kuona yanayoendelea na si kuishia kupokea taarifa, huku akieleza aliyoyatekeleza kwa kipindi chote cha miaka minne.

Sauti ya Mwenyekiti wa Shilabela Fredrick Masalu

Aidha amesema ushirikiano uliopo baina ya wananchi na serikali ya mtaa ndio umesaidia kufanikisha kufikia mafanikio hayo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Shilabela Fredrick Masalu