Storm FM

Shabiki wa Yanga Geita kutoa ngo’mbe 5 kwa wachezaji

7 November 2023, 6:49 pm

Hussein Mwananyanzara shabiki wa Yanga SC mkoani Geita akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Mrisho Sadick.

Kipigo cha Simba kimeendelea kupeleka neema Jangwani baada ya wadau kuanza kujitokeza kutoa zawadi za pongezi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Baada ya Yanga kuifunga Simba goli 5 – 1 shabiki wa Yanga mkoani Geita Hussein Mwananyanzara ameahidi kutoa ng’ombe watano kwa wachezaji na benchi la ufundi la klabu hiyo ili kuwaongezea morali wachezaji hao katika mbio za kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwananyanzara amesema amefikia uamuzi huo baada ya timu yao kuvunja mwiko wa kufungwa na watani wao Simba idadi kubwa ya magoli nakwamba anatoa zawadi hiyo ili kuongeza hamasa.

Sauti ya Mwananyanzara Shabiki wa Yanga