Storm FM

Mtetezi wa mama Chato kusimama na Rais Samia uchaguzi serikali za mitaa

19 January 2024, 12:54 pm

Vijana wa taasisi ya mtetezi wa mama wakiwa kwenye kikao cha kawaida Kata ya Bwanga Chato. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya vijana wilayani Chato wameonesha hisia zao kwa kuungana na Rais Dkt Samia kwa kile walichokieleza kuwa wana imani na serikali yake.

Na Daniel Magwina:

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwaka 2025 vijana wilayani Chato Mkoani Geita wameahidi kumuunga Mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa amefanya kazi kubwa kwa kipindi kifupi kwenye utawala wake.

Vijana hao Kutoka Taasisi ya Mtetezi wa Mama wilayani Chato Mkoani Geita wakiwa kwenye Kata ya Bwanga wilayani humo wamesema hakuna sababu ya kuwaondoa viongozi wa CCM huku wakiahidi kusimama na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa amefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo kuendelea kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda Chato.

Vijana wa taasisi ya mtetezi wa mama wakiwa kwenye kikao cha kawaida Kata ya Bwanga Chato. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya vijana wa taasisi ya Mtetezi wa Mama

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mkoa wa Geita Emmanuel Mgeta amesema wamekubaliana kwa pamoja kumuunga Mkono Rais Dkt Samia pamoja na kutangaza mazuri yake.

Vijana wa taasisi ya mtetezi wa mama wakiwa kwenye kikao cha kawaida Kata ya Bwanga Chato. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mwenyekiti taasisi ya mtetezi wa Mama Geita na Diwani Vitimaalumu Chato