Storm FM
Storm FM
22 June 2026, 8:30 pm

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Geita ametembelea nakukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu ambapo ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Na Mrisho Sadick:
Zaidi ya Shilingi milioni 259 zimetumika kwenye ujenzi wa zahanati katika Vijiji vya Nyabulolo na Imalampaka Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita hatua inayotarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo hayo.
Wakazi wa Vijiji hivyo wakizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kutembelea nakukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo wamesema kukamilika kwa zahanati hizo kutawaondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika maeneo mengine.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Burchard amesema mwezi wa nane mwaka huu miradi hiyo itakuwa imekamilika kwa ubora na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Vijiji hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema Serikali imepanga kutumia bilioni tatu kutoka Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii CSR katika Mgodi wa GGML kukamilisha miradi viporo ya maendeleo ikiwemo maboma ya zahanati, vituo vya afya na miundombinu mingine muhimu.
