Storm FM

Mgusu star yaichapa Kalamata FC mashindano Buhabi Cup

22 July 2026, 6:44 pm

Wachezaji wa Mgusu Star kwenye picha ya pamoja.Picha na Kale Chongela

Mgusu Star ilianza kuifunga Kalamata Fc bao la kwanza katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza na Gori la pili limefugwa dakika ya 65 kipindi cha pili, Gori la tatu limefugwa dakika ya  71.

Na: Kale Chongela

Mashindano ya mpira wa miguu ya Buhabi Cup, yanayodhaminiwa na Diwani wa Kata ya Mgusu, Yohana Yusuph Buhabi, yameanza kwa mchezo wa ufunguzi ulioshuhudia timu ya Mgusu Star ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Kalamata FC kutoka Nyakabale.

Mgusu Star ilianza vyema mchezo huo baada ya Lenard Samweli kuifungia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza, gori la pili limefugwa na Edward Dismasi  dakika ya 65 kipindi cha pili, Gori la tatu limefugwa na  Moses Isaya dakika ya  69  Huku  Ramadhani Huseni  akiiandikia bao la Nne Mgusu stars  dakika ya  71.

Sauti ya Kapteni wa timu ya Mgusu Stars

Mashabiki wa Mgusu Stars na Kalamata Fc wakifuatilia mchezo huo. Picha na Kale Chongela

Hata hivyo, Kalamata FC  Dakika ya 75 imefanikiwa kupata Gori kupitia kwa.mchezaji wao  Shija mwita  na baada ya dakika tisini kukamilika Mgusi Star wameibuka kwa ushindi wa gari  Nne dhidi ya Kalamata  Fc kutoka Nyakambale.

Sauti ya Kapteni wa timu ya Kalamata Fc

Diwani wa kata ya Mgusu Ndugu Yohana Buhabi ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kudumisha upendo kwani michezo ni nyenzo muhimu ya kuunganisha jamii na kuwaepusha vijana na vitendo visivyofaa, huku akiwataka wachezaji, viongozi wa timu na mashabiki kuzingatia nidhamu.

Sauti ya Diwani wa kata ya Mgusu Ndugu Yohana Buhabi

Diwani wa kata ya Mgusu akikagua timu katika mashindano ya Buhabi Cup. Picha na Kale Chongela