Storm FM
Storm FM
21 August 2026, 2:59 pm

Baadhi ya Wakazi wanaolalamikia kuondolewa katika makazi yao.Picha na Edgar Rwenduru
Wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na wamewekeza katika makazi na shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo kuondolewa bila fidia wala kuelekezwa eneo la kwenda kutawaathiri wao na familia zao.
Na: Edga Rwenduru
Wakazi wa Kaya zaidi ya 50 katika Kata ya Bomba Mbili, Manispaa ya Geita wanalalamikia uamuzi wa serikali wa kuwaondoa katika maeneo yao ya makazi waliyoishi kwa zaidi ya miaka 19.
Wakazi hao wamefikia hatua hiyo baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita kuwataka kuondoka katika eneo hilo, wakielezwa kuwa wamejenga na kuishi eneo hilo kinyume na utaratibu.
Wananchi hao wamesema wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na wamewekeza katika makazi na shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo kuondolewa bila fidia wala kuelekezwa eneo la kwenda kutawaathiri wao na familia zao.

Moja ya nyumba inayotakiwa kuondolewa katika Kata ya Bomba Mbili. Picha na Edgar Rwenduru
Akizungumzwa kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Yefred Myenzi ametolea ufafanuzi kuhusu malalamiko hayo ya wakazi wa eneo hilo.
Wakazi hao wanaiomba serikali kuangalia swala hilo kwa kina kwani eneo hilo wanalitegemea kwa makazi na shughuli za kiuchumi.
Ripoti kamili na Edgar Rwenduru