

14 May 2025, 9:31 am
‘Mikopo hii ina riba nafuu kabisa na ni maono ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua wafanyabishara kufikia malengo yao’ – Afisa maendeleo ya Jamii Carlos Gwamgobe
Na: Ester Mabula:
Serikali kupitia wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalumu inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi ili kuwasaidia kuendeleza biashara zao
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mei 13, 2025 katika ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Geita, Afisa maendeleo ya jamii kutoka wizara hiyo Carlos Gwamagobe amesema watakuwa mkoani Geita kwa siku tatu kwa lengo kuu la kuhamasisha wafanyabishara kuweza kujisajili kupata vitambulisho ili kupata mikopo hiyo kwani serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 8 ya mikopo hiyo.
Mwenyekiti wa wafanyabisahara wadogo wadogo maarufu Machinga mkoa wa Geita Maulid Said amesema wafanyabiashara wamehamasika kujisajili ili kupata mikopo lakini changamoto imekuwa ni ucheleweshwaji wa kupewa mikopo hiyo na kushauri changamoto hizo zitatuliwe ili kuweza kurahisisha mchakato huo
Katibu Tawala mkoa wa Geita Mhe. Mohamed Gombati amesema Serikali ya awamu ya sita imeendelea kujipambanua na kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabishara wote na kwamba mikopo hiyo itasiaidia katika kuongeza uchumi wa wafanyabiashara na mkoa kwa ujumla.