Storm FM

Watoto 4 wakamatwa kwa kukesha wakicheza PS

30 May 2021, 2:00 pm

Watoto Wanne(4) Akiwemo  Ramadhani Hasani   Wakazi Wa  Kata Ya Nyankumbu Halmashauri Ya Mji Wa Geita Mkoani Geita Wamekutwa Wamefugiwa Ndani Ya Chumba Cha Mchezo  wa Game za Play Statio PS.

Akielezea Mmoja Wa Wazazi Wa Watoto Hao Bi Amina Jumanne  Amesema Mwanae   Alikutwa Ndani  Akiwa Amefungiwa  Hali Ambayo  Ilimfanya Yeye Awe Na Wasiwasi Juu Ya Mwanae  Kufungiwa Ndani Ya Chumba  Hicho.

Kufuatia  Tukio Hilo Ambalo Limeibua Hofu Kwa Wakazi Wa Eneo Hilo  Baadhi Ya Mashuhuda Wametumia Fursa Hiyo Kuwashauri Wazazi , Walezi  Na Wasimamizi Wa Familia Kuhakikisha Wanasimamia Vyema Watoto Wao  Ili Kuepukana Na Migogoro Isio Kuwa Ya Lazima Katika Jamii

Aidha   Mwenyekiti  Wa Serikali Ya Mtaa Wa Uwanja Bw Enosi Chelehani  Amekiri Kuwepo Kwa Tukio Hilo Katika Mtaa Wake Na Kuwataka  Wamiliki Wa Michezo Ya Bahati Na Sibu Kufika Ofisi Kwake  Ili Kuweza Kutambulika   Katika Mtaa Wake Tofauti Na Hapo Watachukuliwa Hatua Dhidi Yao.

Mwenyekiti wa Mtaa