Storm FM

Vijana msibague kazi

27 April 2021, 2:49 pm

Vijana Mkoani Geita wameshauriwa kuacha tabia ya kubagua kazi na badala yeke wajishughulishe na kazi zozote za halali zenye kuwaingizia kipato.

Chongela na Timoth

Kale Chongela Mwandishi wa Storm FM amepiga Stori na Kijana alieamua kujiajiri kwa utengenezaji wa Bustani na uuzaji wa maua katika halmashauri ya mji wa Geita kazi ambayo imebadilisha maisha yake.

Amesema hakuna maisha bora kama hakuna uwajibikaji, nakuwashauri  vijana Mkoani Geita kuacha uvuvi nakuwajibika katika kazi mbalimbali za halali.

Kale Chongela na Mbunifu wa Bustani