Storm FM

Wazee Mjini Geita Waendelea kumuenzi Dkt John Pombe Magufuli

5 April 2021, 4:36 pm

Baadhi ya wazee katika   Halmashauri ya mji wa Geita   wameomba viongozi mbalimbali kumuenzi Hayati Magufuli  kwa kuwapa kipaumbele kwa huduma mbalimbali za kijamii kama ilivyokuwa enzi za utawala wa  hayati Magufuli .

Wazee hao wamesema kuwa  hayati Magufuli watamkumbuka kwa namna alivyotoa kipaumbele kwa wazee   katika  kusaidiwa na kutatua changamoto ambazo zinawakabili.

Aidha akinamama  wamesema  ni vyema viongozi waliopo madarakani  kuendelea kufuata nyao za hayati Magufuli katika utendaji kazi kwa kuwasilikiza wananchi wao ili kutatua changamoto mbalimbali.