Storm FM

Mabasi mabovu 19 yapigwa stop kusafirisha abiria Geita

24 October 2023, 8:19 pm

Magari ya abiria yakiwa katika Kituo kikuu cha Mabasi Mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kutokana na uwepo wa ajali nyingi mwisho wa mwaka zinazochangiwa na matumizi ya magari mabovu , watu kutozingatia sheria za usalama barabarani , Jeshi la Polisi limekuja na mwarobaini wa matukio hayo.

Na Mrisho Sadick:

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limezuia mabasi 19 ya kusafirisha abiria ndani  na nje ya Mkoa wa Geita kutokana na mabasi hayo kuwa na makosa mbalimbali ya kiufundi hali ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha ya watu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo akizungumzia oparesheni ya ukaguzi wa magari ya abiria. Picha na Mrisho Sadick

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mabasi makubwa na madogo zaidi ya 213 katika kituo kikuu cha mabasi ya abria mjini Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Safia Jongo amesema jeshi hilo limeanza kuchukua hatua kuelekea mwisho wa mwaka ili kukabiliana na changamoto za ajali zinazoweza kudhibitwa nakwamba katika ukaguzi huo mabasi 53 yamekamilika , 142 yamekutwa na makosa yanayorekebishika na mabasi 19 yamezuiliwa.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Katika hatua nyingine Kamanda Jongo amesema Jeshi hilo limeanza msako wa nyumba hadi nyumba kuwasaka wahalifu nakuomba viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti na watendaji kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika oparesheni hiyo. 

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa  Geita Mrakibu  wa Polisi Joachim Aloyse amesema zoezi hilo ni endelevu nakutoa onyo kwa wamiliki na madereva wa mabasi walioficha magari yao kuepuka ukaguzi kuwa wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Sauti ya RTO