Storm FM

Barabara ya Ushirombo-Nyikonga hadi Katoro kuanza kujengwa

10 June 2024, 3:51 pm

Naibu waziri mkuu Dotto Biteko akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika kata ya Katome. Picha na Mrisho Sadick

Serikali imedhamiria katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambazo zimeharibika kutokana na mvua zilizonyesha nchini ili kuweka urahisi kwa wananchi kutumia barabara hizo.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Serikali imeanza mpango wa kujenga barabara ya Ushirombo-Nyikonga mpaka Katoro kwa kiwango cha lami zikiwa ni jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya barabara ambayo kwa kiasi kikubwa imeharibiwa na mvua.

Akiitimisha ziara ya siku tatu Juni 8, 2024 katika jimbo lake la Bukombe Naibu waziri mkuu na mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akiwa ameambatana na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa katika kata ya Katome, Bashungwa alisema barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa rise.

Sauti ya waziri Bashungwa

Aidha Bashungwa ameongeza kuwa serikali itajenga barabara ya njia nne Kutoka mwanza mjini hadi Daraja la JPM linaloendelea kujengwa Busisi ili kuondoa changamoto ya foleni ya magari.

Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika kata ya Katome. Picha na Mrisho Sadick

Naibu wa Waziri mkuu Dkt. Doto Biteko amesema wizara ya ujenzi inahitaji zaidi ya Trioni Moja ili kufanyia marekebisho barabara zote zilizo haribiwa na Mvua.

Sauti ya naibu waziri mkuu Biteko