Storm FM

Wananchi mamlaka ya mji mdogo Katoro walia na TARURA

27 August 2023, 12:33 pm

Picha na Zubeda Handrish

Changamoto ya barabara za mitaa katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro imekuwa ya muda mrefu kiasi cha wananchi wa eneo hilo kuibuka tena na kutoa ya moyoni.

Na Zubeda Handrish- Geita

Baadhi ya wananchi wa kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita, wameiomba serikali kushughulikia changamoto ya daraja pamoja na barabara za mitaa kama Ludete, CCM, Mtaa wa Afya na maeneo mengine hususani mvua zinapoanza kunyesha katika eneo hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa barabara hiyo haijafanyiwa marekebisho kwa miaka mitatu hivyo kusababisha adha kwa waendesha vyombo vya moto, wanafunzi na watembea kwa miguu.

Sauti ya wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wakitoa kero ya ubovu wa barabara.
Sauti ya wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wakitoa kero ya ubovu wa barabara.

Nae Meneja wa TARURA wilaya na mji wa Geita, Eng. Bahati amewataka wananchi kuwa na subira wakati wanafanya jitihada ya kujenga mitaro na barabara, huku akiwataka wanaopaki magari ya kushusha mizigo barabarani kufuata taratatibu.

Meneja wa TARURA wilaya na mji wa Geita, Eng. Bahati.