Storm FM

TRA yawakumbuka watu wenye uhitaji

8 December 2023, 1:50 pm

Maafisa wa TRA wakiwa na maafisa wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Geita mjini. Picha Mrisho Sadick

Jamii imeombwa kuendelea kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu kwakuwa bila kuungana kwa pamoja kuwasaidia wataendelea kuisha katika mazingira magumu.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita imetoa msaada wa Chakula na vitu mbalimbali kwa makundi ya watu wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita.

TRA ikiwa katika maadhimisho ya wiki ya shukrani kwa mlipa kodi imetembelea nakutoa msaada katika kituo cha Kulelea watoto wachanga Cha Neema House, Kituo cha Kulea watoto yatima Cha Moyo wa Huruma ,  Shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya Mbugani na magereza ya wilaya ya Geita huku wasimamizi wa vituo hivyo wakipongeza hatua hiyo.

Sauti ya wasimamizi wa vituo
Maafisa TRA wakitoa msaada katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Moyo wa Huruma Geita mjini . Picha na Mrisho Sadick

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna mkuu wa TRA baada ya kutembelea nakutoa msaada huo wenye thamani ya Shilingi milioni 6, Kamishina wa Kodi za ndani Kutoka makao makuu Alfred Mregi amesema TRA inatambua thamani ya mlipa Kodi nakwamba inawajibu wa kurudisha shukrani kwao.

Sauti ya Kamishna wa Kodi za ndani TRA