Storm FM

Laiza akutwa na chupa zenye mikojo ndani kwake Kivukoni

18 June 2024, 5:50 pm

Muonekano wa chumba cha Laiza ambacho amekuwa akitumia kuhifadhi chupa zenye mikojo ndani. Picha na Edga Rwenduru

Kijana Laiza mkazi wa mtaa wa Kivukoni, kata ya Kalangalala Halmashauri ya Mji wa Geita amekutwa na chupa nyingi zilizotumika zikiwa zimejaa mkojo chumbani kwake.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Akizungumzia tukio hilo Juni 17, 2024 mama mwenye nyumba aishiyo kijana huyo aitwae Marry Masunga amesema walikuwa wakipata harufu mbaya kwa muda mrefu ikitokea katika chumba chake huku wakidhani pengine kuna mtu amefariki.

Sauti ya Marry Masunga
Marry Masunga ambaye ni mama mwenye nyumba. Picha na Edga Rwenduru

Baadhi ya majirani wa kijana huyo ambao ni wapangaji wenzie wameelezea juu ya tukio hilo huku wakieleza kukerwa na harufu hiyo.

Sauti ya majirani

Patrick Paulo ni kamanda wa polisi pamii katika kata ya Kalangalala anaelezea hatua za upokeaji wa taarifa hiyo zilivyokuwa.

Sauti ya kamanda polisi jamii
Mwenyekiti wa mtaa wa Kivukoni Gideon Ally. Picha na Edga Rwenduru

Mwenyekiti wa mtaa huo Gideon Ally amekiri kupokea taarifa ya tukio hilo huku akiwataka wenye nyumba kuzingatia utambulisho wa mpangaji mpya kwa viongozi wa mtaa.

Sauti ya mwenyekiti

Tayari kijana huyo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Geita kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo.