Storm FM

Mtetezi wa Mama yaipongeza serikali kujenga hospitali ya hadhi ya wilaya Katoro

31 July 2023, 4:51 pm

Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Katoro. Picha na Mrisho Sadick

Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwekeza katika huduma za afya kwa kujenga hospitali katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu ikiwemo mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita.

Na Mrisho Sadick:

Wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita wameishukuru serikali kwa kuwajengea hospitali yenye hadhi ya wilaya ambayo imesaidia kupunguza msongamano mkubwa wa watu kwenye kituo cha afya Katoro ambacho kimezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaofika kupatiwa huduma.

Wakizugumza na Storm FM wajumbe wa taasisi ya Mtetezi wa Mama waliofika katika hospital hiyo kufanya usafi wamesema mradi huo umekuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo na kuahidi kuendelea kutangaza mazuri yote yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya wajumbe taasisi ya mtetezi wa mama
Wanachama wa taasisi ya mtetezi wa mama wakifanya usafi Hospitali ya Katoro. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa Mama wilaya ya Geita Elizabeth Coster amesema mradi huo ni mkubwa na hawana budi kuendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusogeza huduma muhimu kwa wananchi huku muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo Faustine Edward amesema huduma zilizoanza kutolewa katika eneo hilo ni huduma za dharura, kina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Sauti ya Mwenyekiti taasisi ya mtetezi wa mama na Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Katoro