Storm FM

Waumini TAG Geita washiriki ujenzi wa Kanisa

16 August 2023, 4:22 am

Kanisa la TAG linalojengwa kwa nguvu ya waumini. Picha na Kale Chongela

Linapokuja suala la kuabudu waumini huwa na moyo na msukumo mkubwa katika utekelezaji wa jambo la kiimani, hili limejiri pia katika Kanisa la Chabulongo.

Na Kale Chongela- Geita

Baadhi ya waumini wa Kanisa la TAG mtaa wa Chabulogo wameshiriki na baadhi ya mafundi katika ujenzi wa Kanisa lililopo katika eneo hilo.

Sauti ya mmoja wa waumini Kanisa la TAG Geita

Wakizungumza na Storm FM wameiambia kuwa wamelazimika kujitoa ili kuhakikisha Viongozi wa dini wanapata sehemu sahihi ya kuwafundisha wananchi neno la Mungu.

Sauti ya mmoja wa waumini Kanisa la TAG Geita

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa hilo la TAG lililopo eneo la Chabulongo Bi. Ester Nyamizi amesema baada ya kuendelea kufanya kazi ya Mungu pamekuwepo na matokea chanya hali ambayo imemlazimu kupanua Kanisa hilo ili washirika waweze kupata sehemu ya kuabudia.

Sauti ya Mchungaji wa Kanisa la TAG Geita