Storm FM

Mashabiki wa soka Geita watamba usajili mpya

11 July 2023, 10:21 pm

Shabiki wa klabu ya Yanga akizungumzia usajili. Picha na Zubeda Handrish

Dirisha kubwa la usajili limefunguliwa rasmi Julai 1, 2023 kwa ajili ya vilabu nchini kuingiza maingizo mapya yatakayowasaidia katika msimu mpya wa 2023/24, huku mapema vilabu hivyo vikianza usajili na kutangaza hadharani wakati vingine vikisajili kimya kimya.

Na Zubeda Handrish – Geita

Mashabiki wa soka Mkoani Geita wamefunguka na kutamba juu ya usajili kwa vilabu vyao wanavyoshabikia na kudai matumaini yao ni makubwa kwa msimu mpya.

Mashabiki wa soka katika egesho la pikipiki la soko la dhahabu. Picha na Zubeda Handrish

Wameyasema hayo ikiwa ni siku 11 tu tangu kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu wa 2023/24 ikiwa ni kwaajili ya Ligi za ndani na michuano ya Kimataifa.

Sauti ya mashabiki wa soka katika egesho la pikipiki la soko la dhahabu mkoani Geita