Storm FM

TRA kuendeleza ushirikiano kwa wanahabari

3 July 2023, 11:43 am

Na Mrisho Sadick

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari kufikisha elimu ya mlipa kodi kwa kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara hususani maeneo ya vijijini hawafikiwi na elimu hiyo mara kwa mara.

Wanahabari Geita
Wanahabari Geita

Kauli hiyo imetolewa na afisa mkuu wa kodi kutoka kitengo cha elimu kwa walipakodi makao makuu  Bi. Lydia Shio katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Geita wa namna mamlaka hiyo inavyotekeleza majukumu yake huku kaimu meneja wa TRA mkoa wa Geita Adam Kobelo akisema waandishi ni kiungo muhimu kati ya mamlaka hiyo na jamii.

Lyidia Shio Afisa Mkuu wa Kodi

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika semina hiyo Renatus Masuguliko na Jane Barnabas wamesema imewasaidia kuwajenga kwa kuwa walikuwa hawajui kwa undani namna mamlaka hiyo inavyofanya kazi kwa kushirikiana na mamlaka zingine za ukusanyaji wa mapato kama halmashauri.

Lyidia Shio Afisa Mkuu wa Kodi