Storm FM

Ulinzi na usalama Geita umeimarika

5 April 2021, 6:35 pm

Na Zubeda Handrish:

Wakazi wa Mtaa wa Msufini mjini Geita wamezungumzia hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao tangu aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuingia madarakani.

Wameyasema hayo walipozungumza na Storm FM na kusema kuwa kwa sasa hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao imeimarika tofauti na kipindi cha nyuma, Pia wamewaasa watanzania kuendelea kumuenzi Hayati Dkt. John Magufuli kwa yale aliyowafanyia watanzania.

Wakazi wa Geita wamesisitizana pia kulindana wao kwa wao na mali zao ili kubaki katika hali ya kiusalama na kila mmoja kuendelea kujivunia kuwa mkazi wa Geita na Tanzania kwa ujumla.